Mwongozo:$wgArticleCountMethod
| Statistics and content analysis: $wgArticleCountMethod | |
|---|---|
| Njia inayotumika kubaini kama ukurasa katika nafasi ya majina ya maudhui unapaswa kuhesabiwa kama ukurasa halali wa maudhui (makala). |
|
| Introduced in version: | 1.18.0 (r88113) |
| Removed in version: | Still in use |
| Allowed values: | (mlolongo wa maandishi) au null |
| Default value: | 'link' (1.24+)null (1.18-1.23) |
| Other settings: Alphabetical | By function | |
Maelezo
Njia inayotumika kubaini kama ukurasa katika nafasi ya majina ya maudhui unapaswa kuhesabiwa kama ukurasa halali wa maudhui (makala).
Kigezo hiki kinaweza kuwa na thamani zifuatazo:
'link'- ukurasa lazima uwe na kiungo cha wiki ili kuzingatiwa kuwa ukurasa halali'comma'- ukurasa lazima uwe na alama ya koma ili kuhesabiwa kuwa halali Kutokana na matatizo ya jinsi chaguo hili lilivyotekelezwa, liliondolewa katika MediaWiki 1.31. Sasa ni sawa na'any'.'any'- kurasa zote (zisizo za uelekezaji) zinachukuliwa kuwa makala halali- Thamani nyingine yoyote itakuwa na matokeo sawa na
'any'.
"Kiungo cha wiki" kilichotajwa hapo juu lazima kiwe kiungo cha aina ya ndani kilichoundwa kwa kutumia [[nafasi mbili za mabano]] (kiungo hiki kinaweza kutolewa na ujumuishaji na hakihitaji kuelekeza kwenye ukurasa uliopo). Viungo hivi huunda rekodi kwenye jedwali la $2, ambalo ndilo linalochunguzwa ili kubaini kama ukurasa una viungo vya wiki. Such links create entries in the pagelinks table, which is what actually gets checked to determine whether a page contains wikilinks.
Aina nyingine za viungo, ikiwemo viungo "vya nje" (vilivyoundwa kwa [bano moja]), viungo vya interwiki (kwenye kurasa za wiki nyingine), viungo vya kategoria (vinavyoweka kurasa kwenye makundi), na viungo vya faili (vinavyonyesha faili) havihesabiki wakati wa kutumia njia ya 'kiungo'.
Kubadilisha kigezo hiki hakutaathiri hesabu zilizopo nyuma. Ili kusasisha, utahitaji kuendesha script ya maintenance/updateArticleCount.php.