Baba yetu
Appearance
The Lord's Prayer in Swahili (Protestant version)
- Baba yetu uliye mbinguni,
- Jina lako litukuzwe,
- Ufalme wako uje,
- Mapenzi yako yatimizwe,
- hapa duniani kama huko mbinguni.
- Utupe leo riziki yetu.
- Utusamehe makosa yetu,
- kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
- Na usitutie majaribuni,
- lakini utuokoe na yule mwovu.
- [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.]
- Amin.
The Lord's Prayer in Swahili (Catholic Version)
- Baba Yetu uliye mbinguni,
- jina lako litukuzwe;
- ufalme wako ufike,
- utakalo lifanyike
- duniani kama mbinguni.
- Utupe leo mkate wetu wa kila siku,
- utusamehe makosa yetu,
- kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea.
- Usitutie katika kishawishi,
- lakini utuopoe maovuni.
- Amina.